Mshambuliaji kutoka nchini Ureno Cristiano Ronaldo atarejea
tena kwenye uwanja wa Old Trafford mjini Manchester mwezi ujao
imethibitika hivyo.
Kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa na mashirikisho ya soka nchini
Ureno pamoja na Argentina imebainika wazi kwamba mshambuliaji huyo
atakuwepo uwanjani hapo kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki
baina ya pande hizo mbili.
Hatua hiyo huenda ikawatuliza baadhi ya mashabiki wa Man Utd
wanaohitaji kumuona Ronaldo akirejea uwanjani hapo akiwa amevaa jezi ya
klabu yao baada ya kufanya hivyo miaka minane iliyopita.
Kikosi cha Ureno ambacho kwa sasa kinaongozwa na mshambuliaji huyo
kama nahodha kitacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki katika uwanja wa
Old Trafford Novemba 18 mwaka huu.
Fursa hiyo itamuwezesha Cristiano Ronaldo kurejea Old Trafford kwa
mara ya pili tangu alipoondoka Man Utd mwaka 2009, na kama itakumbukwa
kwa mara ya kwanza alirejea wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani
Ulaya miaka miwiwli iliyopita akiwa na Real Madrid.
0 comments:
Chapisha Maoni