Alhamisi, Oktoba 30, 2014

AJALI YA CANTER YAUA MBEYA

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Yassini Hezron (14) mkazi wa kiwira alifariki dunia papo hapo baada ya gari lenye namba za usajili T.235 AFP aina ya M/Canter lililokuwa limebeba matofali likiendeshwa na dereva aitwaye Fredy Mpondo kushindwa kupanda mlima na kisha kurudi nyuma na kuangusha matofali na kusababisha kifo kwa tingo huyo.
Ajali hiyo imetokea jana saa 06:00 mchana huko maeneo ya New Land Bar, kata ya Kiwira, tarafa ya Ukukwe, wilaya ya Rungwe, mkoa wa Mbeya katika barabara ya Tukuyu/Kyela. Chanzo cha ajali ni gari hilo kushindwa kupanda mlima na kurudi nyuma. Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu kwa mazishi. Dereva alikimbia mara baada ya tukio hilo na juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa madereva na watumiaji wengine wa vyombo vya moto kuwa makini wanapotumia vyombo hivyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoepukika.
Aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa [dereva] kuzitoa katika mamlaka husika ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

0 comments:

Chapisha Maoni