Jumanne, Septemba 23, 2014

WAFUGAJI ILINGA WATAKIWA KUTUMIA ELIMU

Jamiii ya wafugaji Mkoani Iringa imetakiwa kufuga kwa kuzingatia elimu wanayopewa na maafisa mifugo ili ufugaji wao uwe na tija kwa maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla.
Afisa mifugo wa wilaya ya Iringa Mkoani Iringa Bw.Edward Makyao amesema wafugaji wengi wamekuwa wakifuga kwa njia za asili hali inayopelekea uhalibifu wa mazingira na kutonufaika na ufugaji huo.
Bw.Makyao ameongeza kuwa wanaendelea na utoaji wa elimu kwa wafugaji wa wilaya ya Iringa vijiji katika ufugaji wa mbuzi na kuku wakienyeji ambapo wamewaelimisha juu ya utengenezaji wa banda uchaguzi wa mbegu bora pamoja kutambua magonjwa mbalimbali ambayo huithiri mifugo yao.
Kwa upande wa wafugaji wa Vijiji vya Weru na Kibebe Wilaya ya Iringa Vijijini Mkoani Iringa wameupongeza mpango wa kutolewa kwa elimu hiyo aidha wameitaka serikali kutoa ruzuku ya kupunguza gharama za ununuzi wa vyakula na dawa za kutibu magonjwa ya mifugo yao ikiwa ni pamoja na kuongeza wataalamu wa sekta hiyo hasa maeneo ya vijijini.
Hata hivyo Afisa mifugo Bw.Makyao amesema lengo kuu la elimu hiyo ni kuwafanya wafugaji wafuge kwa kiasi kidogo kwa mavuno mengi zaidi ambapo elimu hiyo inatolewa kwa kushirikiana na shirika la Maendeleo la Mazombe Mahenge (MMADEA) la Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

0 comments:

Chapisha Maoni