SIKU ya Msanii Tanzania inatarajiwa kuadhimishwa Oktoba 25, katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam chini ya kauli ya mbiu yake ya ‘Sanaa ni Kazi.’ Maadhimisho hayo yanayofanyika chini ya uratibu wa Kamati ya Siku ya Msanii kwa ushirikiano na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), yanalenga kuwaunganisha wasanii wa nyanja mbalimbali.
Akizungumza katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, jijini Dar es Salaam jana, Mratibu Mkuu wa Kamati hiyo, Justine Jones, alisema siku hiyo wataungana na wengine duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya msanii.
Alisema maudhui haswa na maadhimisho hayo, ni kumtambua msanii, kazi zake na mchango wake katika jamii.
Alisema fani zinazotarajiwa kutumika katika tukio hilo, ni muziki wa taarabu, muziki wa dansi, ngoma za asili, muziki wa msanii kutoka nje ya nchi, uchezaji shoo, dansi za mitaani, Bongo fleva, maonyesho ya mitindo ya mavazi, semina, sanaa kwa watoto na maonyesho ya sanaa za ufundi.

Kutakuwa na tuzo mbili ambazo tutazitoa kwa msanii aliyejitolea maisha yake yote katika maendeleo ya sanaa (Life Time Achievement Award) na tuzo ya msanii aliyetoa mchango mkubwa katika jamii kupitia sanaa (Huminitarian Award), kwasababu ndio tunaanza kutakuwa na tuzo hizo tu
alisema.
Alisema, tuzo hizo zitatolewa kwa wasanii raia wa Tanzania pekee walio hai na waliokwishafariki ambao wamefanya kazi za sanaa kipindi cha kuanzia mwaka 1964 hadi 3013.
Alisema fomu za tuzo hizo zinaanza kutolewa leo hadi Oktoba 3, ambapo wasanii, jamii na wadau wa sanaa watajaza fomu ili kupendekeza majina ya wasanii wanaostahili kupewa tuzo hizo.

Fomu hizi zinapatika bure katika ofisi za Haak Neel Production Ltd, ofisi za Basata na zinapatikana katika tovuti ya www.haakneelproduction. com, siku ya msanii imedhaminiwa na kampuni ya New Habari (2006) Ltd kupitia magazeti yao ya Bingwa, Dimba, Mtanzania na The African
alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni