Mwalimu mmoja nchini Kenya, ambaye aliibiwa
fedha zake na yeye mwenyewe kupigiliwa msumari kwenye mti, amezungumzia
mkasa huo. Wezi hao walimuibia dola ishirini na nne Peter Asutsa Alhamisi
iliyopita, kabla ya kuupigilia kwa msumari mkono wake kwenye mti katika
msitu mmoja uliopo Eldoret, magharibi mwa Kenya. Mwalimu huyo wa
mafunzo ya Jumapili (Sunday School) alikaa kwa saa kumi na sita akiwa
katika maumivu makali kabla ya kuokolewa na polisi. Amesema aliweza
kuwasiliana na mke wake kwa kutumia simu yake aliyokuwa ameificha kwenye
nguo yake ya ndani. (Picha: | JARED NYATAYA | NATION MEDIA GROUP)




0 comments:
Chapisha Maoni