Ijumaa, Septemba 19, 2014

MAMBO 8 YAKUFANYA UKIWA SAFARINI

1. Kama unakoenda hukujui na ni mgeni upo kituo cha basi unataka kuulizia sehemu fulani basi usijaribu kumuuliza mpitanjia we angalia duka lolote linalo vutia kidogo muulize muuzaji.
2. Kama upo stendi unataka kuchukua daladala/ bodaboda , jitahadi kupiga picha plate namba ya daladala au boda boda itakusaidia.
3. Unapo safari kwenye basi jitahadi kuongea na jirani yako mlie kaa siti moja angalau umjue hata jina wengi wetu huwa hatufanyi hivi kufanya hivyo itakusaidia safari yako itakuwa nzuri sana .
4. Kama una mizigo mabegi basi funga kitambaa kwenye mishikio ya mabegi itakusaidia kuliona begi kwa urahisi kwani wengi hupenda mabegi ya rangi nyeusi unaweza funga kitambaa cha rangi nyekundu au nyeupe.
5. Chagua siti/kiti kilichopo upande wa dereva kwani madereva wengi hutetea sana gari upande aliopo yeye ndiyo maana ni mara chache sana madereva kuumia/ kufa katika ajari.
6. Usiweke nauli mbali sana/kuificha sana wengi tunafanya haya makosa unapanda gari nauli imefichwa sana wakati unajua kuwa unapanda gari la kulipia kufanya hivyo kutakusaidia kutopata usumbufu na kauli za kusema “nimekaa vibaya nitakupa”
7. Jaribu kusoma gazeti au kitabu ukiwa safarini, hii inakusaidia kuto sinzia katika gari na kuongeza maarifa mengine wengi tukiwa safarini tunasinzia kitu ambacho ni hatari kama ikitokea ajari .
8. Hii siyo lazima sana uanaweza mpiga picha konda na plate namba ya gari kama ni la mizigo au gari la lift katika mabasi si lazima kwani hutoa tiketi zenye namba ya gari.

0 comments:

Chapisha Maoni