Jumatano, Septemba 17, 2014

LVG ATOA ZAWADI YA MAGOLI MANNE KWA MKEWE

Meneja wa klabu ya Man utd Aloysius Paulus Maria van Gaal, kwa mara ya kwanza amekiri kuwa na furaha tangu alipoanza kazi nchini Uingereza mara baada ya fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Brazil.
Van Gaal amethibitisha suala la kuwa na furaha baada ya kikosi chake kupata ushindi wa kwanza katika ligi ya nchini Uingereza msimu huu kwa kuibanjua Queens Park Rangers mabao manne kwa sifuri hapo jana.
Van Gaal amesema ushindi huo ni maalum kwake pamoja na wachezaji wote wa Man utd kwa ujumla, kutokana na subra waliyokuwa nayo kwa muda wa majuma matano yaliyopita ambayo yalishuhudia Man Utd ikisemwa na kuandikwa vibaya katika vyombo vya habari.
Pia meneja huyo kutoka nchini Uholanzi ameutunuku ushindi huo wa mabao manne kwa sifuri kwa mke wake mpenzi Truus Van Gaal ambaye mwishoni mwa juma lililopita alikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa.
Katika hatua nyingine Louis Van Gaal amesema ushindi huo unafungua milango ya mafanikio kwa msimu huu kwa kutarajia matokeo mazuri zaidi siku za usoni hivyo amezitaka timu pinzani kukaa mkao wa kupambana na mashetani wekundu.
Van Gaal amesema kabla ya mchezo huo aliwahusia wachezaji wake kutambau hawana budi kucheza kama wanaanza ligi, kutokana na kukifuma upya kikosi chake ambapo aliyatumia baadhi ya majembe aliyoyasajili wakati wa majira ya kiangazi.
Mabao ya Man Utd dhidi ya Queens Park Rangers yalipachikwa wavuni na Angel Fabian Di Maria Hernández, Ander Herrera Aguera, Wayne Mark Rooney pamoja na Juan Manuel Mata Garcia.

0 comments:

Chapisha Maoni