Jumatatu, Septemba 22, 2014

ALICHOKISEMA RPC IRINGA KUHUSU MAANDAMANO YA CHADEMA

Jeshi la polisi limevitaka vyama vya siasa kufuata sheria na taratibu za nchi ili kuimarisha amani na utulivu nchini.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi ametoa wito huo kufuatia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza maandamano na migomo nchi nzima kupinga kuendelea kwa Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma.
Kamanda Mungi amesema vyama vyote vya siasa vipo kwa mujibu wa sheria za nchi hivyo vinapaswa kufuata ili kuepusha migogoro.
Amesema sheria inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano na maandamano kwa kufuata sheria ikiwemo kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili kupata kibali kwa ajili ya usalama.
Kamanda Mungi amesema jeshi la polisi limejipanga vizuri kuzuia na kupambana na vitendo vya uvunjifu wa amani kwa wananchi.
Hata hivyo, kamanda wa polisi mkoa wa Iringa amewataka wananchi kufanya kazi za uzalishaji mali kwa ajili ya maendeleo na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani.

0 comments:

Chapisha Maoni