Jumanne, Septemba 02, 2014

AJIUA BAADA YA KUUGUA TB 18

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Butungo Mbugani mkazi wa kitongoji cha Ntegele kijiji cha Igulwa kata hiyo wilayani Bukombe mkoani Geita amechukua jukumu la kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani baada kuugua kwa muda wa miaka 18 ugonjwa wa kifua kikuu (TB) kwa mujibu wa sungwakareny.blogspot.com.
Kijana huyo ambaye alianza kuugua maradhi hayo akiwa na umri wa miaka miwili alishindwa kupona na badala yake alichukua uamuzi wa kujinyonga huku akiacha ujumbe ulioandikwa kwenye karatasi kuwa
kwa heri baba nimeamua kujinyonga sababu ya kuugua muda mrefu nakwenda kuanza maisha mapya ahera.
Kwa mujibu wa maelezo ya baba wa marehemu Mbugani Maleka alisema kuwa mwanaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo tangu akiwa na umri wa miaka miwili na kumfanya asisome ,ambapo alieleza kuwa kifo hicho kimekuwa na mshtuko mkubwa kwani hawakufikiria kama angechukua uamuzi huo.
Alisema katika uhai wake licha ya kuugua muda mrefu alikuwa akitibiwa katika hospitali ya wilaya ya Bukombe na vituo vya afya tofauti tofauti na kupata unafuu ikiwa ilimfanya dawa alizokuwa akipewa kuendeleza hata shughuli zake ili kuweza kujipatia kipato.
Ofisa mtendaji wa kijiji hicho Andrew Tungu baada ya kupata taarifa majira ya saa 4 asubuhi kwa kutokea kifo hicho alisema kuwa baadhi ya wananchi wenye maradhi ya kusumbua muda mrefu wanatakiwa kumuona mtaalamu mara kwa mara na sio kuchukua jukumu zito kama hilo huku akiwataka wazazi na walezi kuzingatia chanjo maalumu kwa watoto na sio kupuuza.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita Joseph Konyo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji hicho ambapo alieleza kuwa fiko cha kijana huyo kinatakiwa kuchunguzwa kitaalamu zaidi .

0 comments:

Chapisha Maoni