Jumatatu, Agosti 11, 2014

WATATU WAFA KATIKA MATUKIO MATATU TOFAUTI IRINGA

Watu watatu wamefariki mkoani Iringa  katika matukio tofauti likiwemo la kufyatuliwa bunduki aina ya gobole.Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa Bw. Ramadhani Mungi  amewataja waliofariki kuwa ni Peter Mfilinge miaka 71  mkazi wa kiponzero ,Harrison  Lugenge miaka 41 mkazi wa kihesa pamoja na Shiriki Katinga miaka 23 mkazi wa Isanga.
BW. Mungi akiongea na Fichuo Tz amesema chanzo vifo hivo ni  uzembe wa madereva kuendesha gari bila kufuata kanuni na taratibu za barabarani pamoja na  umiliki wa siraha  kinyume na sheria.
Aidha  katika tukio lingine jeshi la polisi linawashikilia  watu wanne  kwa tuhumiwa  mbalimbali ikiwemo  kukutwa na risasi aina ya gobole , madawa ya kulevya pamoja na kusababisha ajali.
Hata hivyo, Kamanda wa jeshi la polisi  mkoa wa Iringa amesema wanaowashikilia ni Aida Kikoti miaka 35,Riziki Paskal miaka 16, na Godfrey mbonde miaka 27 wote wakazi wakazi wa Iringa. 

0 comments:

Chapisha Maoni