Naamini kwamba kila mmoja wetu hapa anajua ni jinsi gani ilivyo ngumu
kupata kazi. Hivi sasa imezoeleka kabisa kuwa kupata kazi ni lazima
ubebwe, au uwe na ndugu yako mkubwa serikalini atakayekupa ki memo ili
uweze kupata kazi bila kupitia tanuru la moto.
Hali hiyo imesababisha watu wengi hata wakiona tangazo la ajira kukata tamaa hata kabla ya kupeleka maombi yao ya kazi. Lakini pia sifa zinazotakiwa ili kujaza nafasi hazitoi nafasi kwa watafutaji wengi wa kazi na hivyo wengi hulazimika kudanganya
Hapa chini nitataja baadhi ya point za uongo unaosemwa na watu wanaoomba kazi ili angalau wapate kazi:
1. Mimi nina uzoefu wa kufanya kazi zaidi ya moja kwa wakati mmoja - Huu
ni uongo wa dhahiri, wengi wetu tunadanganya sana kuhusu hili, wakati
hata tukipewa kazi mbili tu tunaaanza kulalamika kwamba tunaonewa.Hali hiyo imesababisha watu wengi hata wakiona tangazo la ajira kukata tamaa hata kabla ya kupeleka maombi yao ya kazi. Lakini pia sifa zinazotakiwa ili kujaza nafasi hazitoi nafasi kwa watafutaji wengi wa kazi na hivyo wengi hulazimika kudanganya
Hapa chini nitataja baadhi ya point za uongo unaosemwa na watu wanaoomba kazi ili angalau wapate kazi:
2. Napenda sana changamoto na huwa sikati tamaa wakati ninapokumbana na changamotoI kwenye kazi yangu – Mh! uongo wa mchana kweupe. Na kwa bahati mbaya unaweza kukuta watu wote waliofanyiwa usaili wametoa kauli hiyo, hivi inawezekana kweli wote muwe mnapenda changamoto wakati wengine changamoto, ndogo tu wananawa mikono na kusalimu amri mpaka wapate msaada
3. Mimi ni kijana ninayekaribia miaka 30 na sijaoa (Kwa wanaume wengi) - Unaweza kuta anakaribia miaka 40 na anaishi na hawara na watoto kila kona aliozaa na wanawake tofauti tofauti. siku hizi umri mkubwa ni kikwazo makampuni mengi yanakimbilia vijana ambao bado hajaoa na hawana majukumu, sasa ili kupata kazi wengi hudanganya kuhusu hilo.
4. Nilikuwa natamani sana siku moja itokee nifanye kazi na kampuni hii - Uongo mwingine tena, unaweza kukuta wengine hata jina la hiyo kampuni walilijua siku hiyo walipoona tangazo la kazi.
5. Kwangu mimi mshahara siyo kipaumbele changu, niko tayari kufanya kazi kwa mshahara wowote mtakaonipa - Kweli? Wakati wengine hukimbilia hapa JF kuulizia kiwango cha mshahara wa taaluma fulani katika kampuni anayoomba kazi......
6. Mimi naweza kufanya kazi katika timu - Wakati wengine kazi yao majungu na kuwagawa watu ndiyo vipaji vyao.
7. Niliacha kazi katika kampuni yangu ya awali kwa ridhaa yangu mwenyewe ili nipate fursa ya kutafuta kazi itakayoipa uzoefu zaidi - Nyoooo... Labda HR wa kampuni ulipotoka asije ulizwa, uliona lini mtu akaacha kazi kabla ya kupata kazi, je utaishije kabla ya kupata kazi nyingine?
0 comments:
Chapisha Maoni