Jumatatu, Agosti 04, 2014

BUNGE LA KATIBA KUENDELEA KESHO BILA YA UKAWA

Bunge Maalumu la Katiba litaendelea na vikao bila kujali uwepo au kutokuwapo kwa baadhi ya wajumbe waliojiundia kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, ambaye ndiye Mratibu wa Bunge hilo, alitoa kauli hiyo jana wakati wa mdahalo ulioandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa).
Alikuwa akijibu hoja iliyowasilishwa wa wachangia mada mbalimbali, kuhusu kusitishwa kwa Bunge hilo kupisha Uchaguzi Mkuu ufanyike, kisha mchakato uanze upya katika Serikali ya Awamu ya Tano.
Hoja nyingine kama hiyo ambayo Lukuvi aliitolea jibu hilo, ni ya kusogezwa mbele kwa Bunge Maalumu la Katiba, ili kutoa muda kama wa wiki moja wa kushawishi zaidi wajumbe wa Ukawa, kurejea katika Bunge hilo.
Ukawa wasipofika bungeni hatutasitisha Bunge, tuliopo tunatosha, tutajadilina na kufikia makubaliano na kuja kuwaeleza wananchi ingawa haitakuwa na afya sana
alisema Lukuvi katika mdahalo huo ambao mada ilikuwa ‘Nini kifanyike Bunge Maalumu la Katiba liendelee’.

0 comments:

Chapisha Maoni