Siku kama ya leo miaka 54
iliyopita, Jamhuri ya Afrika ya Kati ilijikomboa na kupata uhuru toka
kwa mkoloni Mfaransa. Ilikuwa katikati ya karne ya 19 wakati nchi hiyo
iliyokuwa ikijulikana hapo kabla kwa jina la Ubangi-Shari,
ilipounganishwa na makoloni ya Ufaransa barani Afrika. Hata hivyo mwaka
1958, Jamhuri ya Afrika ya Kati ilijipatia Mamlaka ya Ndani na miaka
miwili baadaye yaani mwaka 1960, ikajikomboa na kupata uhuru kamili.
Katika siku kama ya leo miaka
36 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria Shamsiya, maandamano makubwa
yalifanyika katika mji wa Esfahan nchini Iran, baada ya kupamba moto
harakati za mapambano za wananchi Waislamu dhidi ya utawala wa Shah. Kwa
utaratibu huo, wananchi wa mji huo waliingia kikamilifu katika harakati
za mapambano za kutaka kuuangusha utawala dhalimu wa Mfalme Shah.
Maandamano na harakati za wananchi wa Esfahan zilikuwa na umuhimu mkubwa
kiasi kwamba, utawala wa Mfalme Shah uliingiwa na hofu na wahaka mkubwa
hali iliyoufanya uanzishe serikali ya kijeshi mjini humo.
Na tarehe 13 Agosti miaka 115
iliyopita alizaliwa Alfred Hitchcock mtengeneza filamu mashuhuri wa
Kiingereza. Alionesha kazi yake ya kwanza mwaka 1920 na baadaye akaanza
kujihusisha na uongozaji filamu. Filamu zake za kuogopesha na za
kusisimua zilikuwa mashuhuri mno katika zama hizo. Filamu hizo
zilimfanya awe mashuhuri kwa jina la the Master of Suspense. Miongoni
mwa filamu zake ni The Man Who Knew Too Much na Young and Innocent.
Alfred Hitchcock aliaga dunia tarehe 28 Aprili 1980.




0 comments:
Chapisha Maoni