Jumatatu, Agosti 04, 2014

MSIMAMO WA CUF KUHUSU USHIRIKI WAO KATIKA BUNGE LA KATIBA

YAH: KUTOSHIRIKI AWAMU YA PILI YA BUNGE MAALUM LA KATIBA.

Tafadhali husika na somo hapo juu.


Mtakumbuka kuwa Chama chetu kwa kushirikiana na vyama vingine vinavyoounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) tuliamua kutoka katika Bunge maalum la Katiba baada ya CCM kuamua kukiuka utaratibu wa mchakato wa kupata katiba mpya kama ulivyoainishwa katika sheria ya mabadiliko ya Katiba na kuweka Mkakati wa kupitisha Rasimu ya CCM ya serikali mbili.
Pamoja na juhudi ambazo tumeendelea kuzifanya kama Chama na UKAWA, hadi sasa bado CCM wanaonekana hawana dhamira ya dhati ya kuurejesha mjadala wa Katiba Mpya kwa kuheshimu maoni ya wananchi kama yalivyoratibiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuwekwa katika Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa katika Bunge Maalum.

Kwa barua hii, Wabunge wote wa Bunge Maalum la Katiba tunaotokana na Chama cha CUF tunajulishwa kutokwenda kushiriki katika kikao cha awamu ya pili ya Bunge hilo kinachotarajiwa kuanza tarehe 05/08/2014.
Kama Chama kinachoheshimu Demokrasia ya kweli, hatuwezi kushiriki na kuvipa uhalali vikao vya Bunge Maalum vyenye lengo la kuyapuuza na kuyatupilia mbali maoni ya Wananchi.
Nawatakia kila la heri,

HAKI SAWA KWA WOTE
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti Taifa.

NB Ikumbukwe wajumbe hawa wa Cuf ndio wenye thelithi mbili ili CCM ipitishe katiba inahitaji wajumbe 16 toka Cuf, nauo ndio msimamo makini wa Mchumi bingwa duniani KAZI IPO kwa JK mwaka huu. 

0 comments:

Chapisha Maoni