Taarifa ikufikie kwamba wanaume tata ambao si riziki (mashoga) na wanawake wanaojishughulisha na mapenzi ya jinsi moja (wasagaji) kutoka nchi mbalimbali wamefanya mkutano wao mkubwa wa kimataifa jijini Dar.
Tukio hilo lilifanyika kwa siku tatu mfululizo mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli maarufu iliyopo Posta jijini Dar wakitaka serikali ya Tanzania itambue na kuhalalisha mapenzi hayo ya jinsi moja na ikiwezekana hata katiba mpya inayotaka kuundwa sasa hivi viingizwe vipengele vinavyowahusu wao.
Bila kujua anazungumza na mwanahabari wetu, mmoja wao alipoulizwa nini kinaendelea hotelini hapo, alisema mkutano huo unawahusu mashoga na wasagaji huku akibainisha kwamba unafanywa kwa siri kubwa.
Baada ya kupata taarifa hizo, chanzo kiliingia ndani kimafia ambapo kilinasa mazungumzo ya kikao hicho, ajenda kubwa ikiwa ni kuishinikiza serikali itambue uwepo wao hapa nchini.
Ili kujua kama wizara inajua kinachoendelea, chanzo kilimtafuta Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba lakini simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea.
Ili kujua kama wizara inajua kinachoendelea, chanzo kilimtafuta Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba lakini simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea.
0 comments:
Chapisha Maoni