Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Cecilia Hamis (pichani),
mkazi wa Majoe Mjimpya Relini jijini Dar es Salaam amemlalamikia mumewe
aliyemtaja kwa jina la Hamis Juma kwamba ametembea na mbwa wao mweusi
hadi kumpa mimba.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake, mwanamke huyo alisema alibaini hilo wiki mbili zilizopita.
Nililigundua hilo wiki mbili zilizopita. Nakumbuka ilikuwa usiku nikiwa nimelala, nikamsikia mbwa mmoja (kati ya wawili) analia. Niliamka kwenda kuangalia ili kujua sababu, kufika nikawasha tochi ya simu, nilishangaa sana kumwona mume wangu yuko naye amemshikilia mbwa huyo akifanya nae mapenzi!
Nilimuuliza anachokifanya, akasema anammalizia shida zake kwa kuwa hakuna mbwa wa kiume wa kumsaidia
alisema mwanamke huyo.Akiendelea kumlalamikia mume wake kwa madai hayo mazito, mama huyo alisema:
Siku iliyofuata usiku tena, nikiwa nimelala nilimsikia mbwa akilia, nikaamka. Safari hii niliambatana na watoto wangu, tukaenda nje, kufika tukamshuhudia mume wangu akifanya tukio kama la jana yake, nilipomuuliza akanipa majibu yaleyale kwamba anammaliza shida zake mbwa huyo.
Akaendelea:
Hawa mbwa waliletwa wawili wakiwa wadogo kabisa na wote ni majike na tangu walipoletwa sijawahi kumwona mbwa dume hata siku moja kwani mara nyingi tunawafungia kwenye banda lao.
Na tangu mume wangu aanze mchezo huo huyo mbwa mmoja mweusi (pichani) amenawiri kupita kiasi, naamini amempa mimba.
Mwanamke
huyo alisema kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo, aliamua kuwaeleza
majirani ambao nao walimshauri aende kuripoti kwa mjumbe wa eneo hilo.
Mjumbe
wa Shina Na. 26, Majoe Mjimpya, Mbaruka Nyamaishwa alikiri kupokea
malalamiko hayo kutoka kwa mwanamke huyo akamshauri kuyapeleka kwenye
Kituo cha Polisi cha Stakishari.
Habari zaidi zinawekwa wazi kwamba,
majirani nao walipoona mwanamke huyo anachelewa kwenda polisi, wao
walimsomba na kwenda naye ambapo walitoa taarifa katika Dawati la
Jinsia.
Mkuu wa dawati hilo, Koplo Golbert aliongozana na walalamikaji hao hadi nyumbani kwa mdaiwa ambapo alimkagua mbwa huyo na kuwaamuru wanandoa hao kuripoti kwenye kituo hicho cha polisi bila kukosa jana Jumatatu saa 3 kuonana na mkuu huyo na uchunguzi kuendelea.
Mkuu wa dawati hilo, Koplo Golbert aliongozana na walalamikaji hao hadi nyumbani kwa mdaiwa ambapo alimkagua mbwa huyo na kuwaamuru wanandoa hao kuripoti kwenye kituo hicho cha polisi bila kukosa jana Jumatatu saa 3 kuonana na mkuu huyo na uchunguzi kuendelea.
ALICHOKISEMA DAKTARI WA MUHIMBILI
Chanzo cha habari hii kilitilia shaka uwezekano wa mbwa kunasa mimba ya binadamu, hivyo lilimsaka daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kumuuliza kuhusu madai ya mwanamke huyo.
Msikie:
Chanzo cha habari hii kilitilia shaka uwezekano wa mbwa kunasa mimba ya binadamu, hivyo lilimsaka daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kumuuliza kuhusu madai ya mwanamke huyo.
Msikie:
Mh! Binadamu kumpa mimba mbwa haiwezekani. Binadamu anaweza kumpa mimba sokwe, kwa mbali sana nyani. Lakini si mbwa.
Ila kama huyo mama anasema hivyo, mbwa akapimwe na ikibainika ni kweli basi yatakuwa maajabu ya dunia maana dunia ina mambo yake.
0 comments:
Chapisha Maoni