Alhamisi, Agosti 07, 2014

MANENO YA ZITTO KUHUSU MSIMAMO WAKE JUU YA BUNGE LA KATIBA


Katiba ya nchi haiwezi kuandikwa bila maridhiano ya makundi yote. Sitakwenda Dodoma licha ya ushauri mbalimbali kwamba nikasemee ndani. Nitakwenda kwenye Bunge la Katiba pale tu nitakaporidhika kuwa kuna maridhiano baina ya makundi na wadau. Ushauri wangu ni kusitisha Bunge Maalumu na kukubaliana maeneo kadhaa ya kurekebisha katika Katiba ya sasa kisha tupate muda wenye utulivu baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 ili kuandika Katiba Bora. Umoja wa Katiba Bora yenye ridhaa ya wananchi ndio kupona kwa nchi yetu dhidi ya machafuko. Wenye kudhani Katiba ni sawa na ushabiki wa Simba na Yanga wasubiri Ligi Kuu ianze waende Uwanjani kushabikia.

0 comments:

Chapisha Maoni