Alhamisi, Agosti 28, 2014

KUHUSU MSAADA WA UVCCM IRINGA

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa umetoa msaada wa vitu mbalimbali kwenye hospitari ya Mkoa wa Iringa kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa Bi.Tumaini Msowoya amesema watoto ni vijana wa kesho hivyo kuwasaidia wakiwa wadogo ni maandalizi ya kulijenga taifa lenye nguvu kwa maendeleo ya chama na taifa kwa ujumla.
Nao baadhi ya wazazi wa watoto hao wameshukuru kuupata msaada huo ambao ni sabuni,miswaki na dawa za meno ambapo wamewaomba viongozi wengine na asasi mbalimbali kuwa na moyo wa kuwatembelea wagojwa wenye mahitaji mbalimbali.
Kwa upande wa dkt.Aizack Mlai amesema changamoto kubwa inayokabili wodi ya watoto hospitari ya Mkoa wa Iringa ni kukosekana kwa madawa ya kutosha pamoja na vifaa mbalimbali aidha amewaasa wazazi kuwa makini kutokana na mlipuko wa magonjwa ya kuhara,kutapika na malaria.
Hata hivyo Mwenyekiti wa UVCCM amesema baada ya kutembelea wodi ya watoto wanampango wa kuyatembelea makundi ya watu mbalimbali yenye mahitaji maalumu wakiwepo wazee,walemavu na wafungwa magerezani.

0 comments:

Chapisha Maoni