Jumanne, Agosti 05, 2014

KILICHOFANYWA NA SHABIKI WA LIVERPOOL NI ZAIDI YA KITUKO

Shabiki wa klabu ya Liverpool aliyekuwa mmoja wa mashuhuda wa mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya Champions Cup uliochezwa nchini Marekani mapema hii leo, ameacha kibweka nchini humo baada ya kuvaa flana ambayo inakebehi kitendo cha utovu wa nidhamu kilichoonyeshwa na aliyekuwa mshambuliaji wa klabu hiyo Luis Suarez, wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka huu zilizochezwa nchini Brazil.
Shabiki huyo mwanadada alionekana akiwa amevalia flana yenye maandishi yaliyosomeka “Suarez Was Here” akimaanisha “Suarez alikuwepo hapa” na sehemu ya bega lake pameokana na tundu lililonakshiwa sehemu ya memo.
Hata hivyo shabiki huyo hakuonekana kujali sana licha ya kuvaa flana hiyo ambayo iliwakumbusha mbali mashabiki wenzake ambao alikuwa amekaanao jukwani wakifuatilia mchezo wa Man Utd dhidi ya Liverpool.
Kama itakumbukwa vyema Luis Suarez kwa sasa anakabiliwa na kifungo cha kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa miezi minne, baada ya kubainika alimng’ata kwa makusudi beki wa timu ya taifa ya Italia Georgio Chiellini

0 comments:

Chapisha Maoni