Jumatano, Agosti 27, 2014

KARRUECHE TRAN AOMBA RADHI BAADA YA KUMDIS BLUE IVY, MTOTO WA JAY Z

Karrueche Tran amewaomba radhi mashabiki wa Beyonce waliomshambulia kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudiss muonekano wa nywele za Blue Ivy kwenye tuzo za MTV VMAs, wakati akifanya kipindi cha 106& Park cha BET.
Karrueche aliponda muonekano wa nywele za Blue Ivy katika kipengele cha kipindi hicho kilichopewa jina la ‘Top 6 Things Blue Ivy thought about the VMA’s’, ambapo alisikika akisema kwa kumkariri Blue Ivy kuwa ‘Kweli niliamka hivi kwa sababu wazazi wangu hawakunichana nywele. Pole Blue! Nakupenda!”
Mashambulizi yaliyoendelea ndani ya siku mbili mfululizo yamemfanya mrembo huyo kuomba radhi kupitia Instagram akikiri kufanya makosa kwa kuwa yeye ni binadamu.
Katika maelezo yake, ameomba radhi kwa kutamka sentensi hiyo ambayo amesema ilitengenezwa kwenye muongozo wa kipindi na BET na ikapitia kwake.
BET wamewajibika pia na kueleza kuwa Karrueche alikuwa anasoma maelezo hayo kwenye teleprompter (screen ya kusomea habari kwenye TV) kama sehemu ya script na kwamba ilifanyiwa mabadiliko dakika kumi kabla ya kwenda hewani na hakupata nafasi ya kuipitia tena. Huenda angekataa kuisoma kama angeipitia awali.

0 comments:

Chapisha Maoni