Jumapili, Agosti 31, 2014

HII NDIO NCHI NYINGINE YA AFRIKA ILIYOVAMIWA NA EBOLA

Waziri wa Afya wa Senegal amethibitisha kua ugonjwa wa Ebola umekwisha tua nchini mwake na kufanya hesabu ya kua nchi ya kumi na tano kutoka Africa magharibi kukumbwa na ugonjwa huo .
Mwishoni mwa wiki waziri huyo Awa Marie Coll Seck aliwaambia waandishi habari kwamba kijana mmoja kutoka Guinea aliingia nchini Senegal akiwa ameshaambukizwa ugonjwa wa Ebola, na alipogunduliwa, mara moja aliwekwa katika karantini.
Mripuko wa hivi karibuni ulitokea nchini Guinea, umeua Zaidi ya watu 1,500 .
Na wengine 3,000 waliambukizwa virusi vya ugonjwa huo nalo shirika la afya duniani limeonya kua hali inaweza kuwa mbaya Zaidi na huenda ukaambukiza watu wengine Zaidi ya 20,000 people.
Kutokana na kutambuliwa kwa mgonjwa huyo Senegal imefunga mipaka yake na nchi ya Guinea ili kuepusha kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.

0 comments:

Chapisha Maoni