Mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yupo katika uchunguzi wa hali ya juu, habari
zinadai kwamba kila anaponyanyua miguu, kikosi cha kupambana na kuzuia
madawa ya kulevya nchini chini ya kamishna wake, Godfrey Nzowa nao
wananyanyua miguu yao kumfuatilia.
Habari za kiintelijensia zilidai kwamba, kisa cha kikosi hicho
kufanya hivyo kinadaiwa kuwa, serikali inamhofia kujihusisha na biashara
hiyo haramu ya kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ nje ya nchi kwa
kutumia kivuli cha kwenda kufanya shoo.
Akizungumza na wanahabari wetu jijini Dar, Jumatatu iliyopita, afisa mmoja wa ngazi ya juu wa kitengo hicho ambaye hakupenda jina lake liandikwe mtandaoni, alisema Diamond amepewa maelekezo yote muhimu.
Tumempa maelekezo Diamond, atuletee mikataba ya shoo zote anazokwenda kuzifanya nje ya nchi ili tujiridhishe kama kweli ni halali au anakwenda kwa ajili ya biashara nyingine.
Hiyo yote inatokana na uchunguzi wetu kwake kuhusu akaunti zake za benki kuonesha kwamba ana fedha nyingi sana zinazotia shaka kama amezipata kihalali
alisema afisa huyo.
Afisa huyo aliendelea kusema kwamba, uchunguzi wao pia umebaini
kwamba, msanii huyo wa Bongo amekuwa akinunua nyumba kila anaporejea
kutoka kwenye shoo zake nje ya nchi, jambo ambalo taasisi haiamini kama
kweli analipwa pesa nyingi kwa shoo moja, kiasi cha kumwezesha kununua
nyumba jijini Dar.
Tumebaini kwamba Diamond kila akirudi nchini kutoka kwenye shoo zake hununua nyumba. Analipwa kiasi gani cha fedha kule kwenye shoo? Hapa ndipo tunaposimamia sisi
alisema afisa huyo huku akigongea msumari
kuwa Diamond mwenyewe amekatazwa kuzungumza kwenye vyombo vya habari
kuhusu kutakiwa kuwasilisha mikataba ya shoo zake za nje.
Uchunguzi wa Fichuo umepata ukweli kwamba, Diamond aliporejea kutoka kwenye
safari yake ya Marekani hivi karibuni, alinunua nyumba kwa Sh. milioni
80 iliyopo maeneo ya Mwananyamala-Magengeni, Dar.
Siku za nyuma, msanii huyo aliwahi kuripotiwa kununua nyumba zaidi ya mbili maeneo ya Kijitonyama, Dar, kiasi cha kuandikwa na vyombo vya habari kwamba amenunua mtaa.
Siku za nyuma, msanii huyo aliwahi kuripotiwa kununua nyumba zaidi ya mbili maeneo ya Kijitonyama, Dar, kiasi cha kuandikwa na vyombo vya habari kwamba amenunua mtaa.
Diamond mwenyewe aliwahi kuhojiwa katika Kipindi cha Take-One
kinachorushwa hewani na CloudsTV ambapo alipoulizwa akaunti yake
inasomaje, alijibu kuwa ina zaidi ya bilioni moja hivi.
DONDOO ZA UWEZO WA DIAMOND
1. Ana utajiri unaozidi shilingi bilioni 1.
2. Yupo kwenye mazungumzo na promota wa Rwanda kufanya shoo moja ya uwanjani ambayo anaweza kulipwa dola 120,000 (zaidi ya Sh. milioni 190).
1. Ana utajiri unaozidi shilingi bilioni 1.
2. Yupo kwenye mazungumzo na promota wa Rwanda kufanya shoo moja ya uwanjani ambayo anaweza kulipwa dola 120,000 (zaidi ya Sh. milioni 190).
3. Malipo ambayo hupokea kwa shoo zake nyingi za nje ya nchi hayashuki chini ya dola 25,000 (zaidi ya Sh. milioni 40).
4. Tangu mwaka 2011 mwishoni akaunti yake haijawahi kushuka chini ya Sh. milioni 100.
5. Anamiliki nyumba kadhaa jijini Dar ambazo amepangisha watu.
6. Ili kuvunja mkataba na aliyekuwa meneja wake, Papa Misifa ilibidi amlipe Sh. milioni 18.
4. Tangu mwaka 2011 mwishoni akaunti yake haijawahi kushuka chini ya Sh. milioni 100.
5. Anamiliki nyumba kadhaa jijini Dar ambazo amepangisha watu.
6. Ili kuvunja mkataba na aliyekuwa meneja wake, Papa Misifa ilibidi amlipe Sh. milioni 18.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya
Tanzania, Nzowa amesema:
Ni kweli! Sisi kila mtu mwenye kipato cha kutia shaka lazima tumchunguze. Diamond kama ana mali zote kwa nini tusimchunguze. Ikithibitika anajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ama zake ama zetu huo ndiyo utaratibu wetu.
Chanzo kilimsaka Diamond na kumuuliza kama analijua kasheshe hilo ambapo alisema:
Najua, ila nimegundua kuna watu wamepanga kunishusha chini kisanii ndiyo wanaoeneza taarifa kwamba mimi nasafirisha unga. We elewe hivyo kaka (akakata simu).
Kwa kipindi kirefu sasa Diamond
ambaye ni mpenzi wa Wema Isaac Sepetu, amekuwa akisafiri nchi mbalimbali
kwa shoo na mambo binafsi ambapo mbali na nchi kibao za Bara la Afrika,
ameshasafiri nchi nyingi zikiwemo Marekani, Uingereza, China, Norway,
Ujerumani, Dubai na nyinginezo.




0 comments:
Chapisha Maoni