Ukatili dhidi ya wenye ulemavu wa ngozi (Albino) umejitokeza tena
mkoani Tabora ambapo mtoto Pendo Sengerema (14) mwanafunzi wa darasa la
sita shule ya msingi Nundu, amekatwa mkoni wake wa kulia na wahalifu
kukimia nao kusikojulikana na aliyeshiriki uharifu huo akihaidiwa
kulipwa laki tisa huko katika kijiji cha Usinge wilayani Kaliua.
Akiongea kwa tabu alipolazwa katika hospitali ya wilaya ya Urambo
majeruhi Pendo Sengerema amesema kuwa, aliyemkata mkono alimfahamu
maana ni jirani anayesadikiwa kuwa, ni mganga wa kienyeji, ambapo kaimu
mganga wa hospitali hiyo, Doct James Kang’oma, akidai kuwa walijitahidi
kuokoa maisha yake kutokanana kutoka kuvuja damu nyingi.
Mratibu wa chama cha wenye ulemavu wa ngozi wilaya za Urambo na
Kaliua Bw Focus Mgesera, amesema kuwa, pamoja na mtoto huyo kulazwa
katika hospitali hiyo bado kuna hali ya hatali kwake kwani kwa namna
moja ama nyingine anaweza kuuawa kutokana na kuwafahamu waliomjeruhi,
hivyo anahitaji ulinzi.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Under the same sun, Bi Vicky
Ntetemya aliyefika hospitalini hapo kumwona mtoto huyo amesema kuwa,
serikali iwe makini na jamii ya wenye ulemavu wa ngozi kutokana na
masuala ya wagombea nafasi za uongozi kujishirikisha ma mambo ya waganga
wa kienyeji.
Chama cha walemavu wa ngozi nchini kimeraani tukio hilo kikitaka
serikali kuongeza ulinzi kwa jamii hiyo ambapo akizungumza kwa njia ya
simu, kamanda wa polisi mkoani Tabora Suzan Kaganda akidhibitisha
kutokeaa tukio hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni