Jumatano, Julai 02, 2014

UTAJIRI WA LOWASA HUU HAPA

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema madai kwamba yeye ni tajiri hayana ukweli wowote. Amesema yeye ni mfugaji na anamiliki ng’ombe zaidi ya 800 katika Jimbo la Monduli, mkoani Arusha.
Lowassa alisema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisini kwake wiki iliyopita mjini Dodoma.
Haya madai hayana hata chembe ya ukweli hata kidogo, isipokuwa mimi nadhani wananitakia mema kwa sababu ukiona jumba zuri wanasema la Lowassa, gari nzuri la Lowassa, kitu chochote kizuri wanasema cha Lowassa
alisema na kuongeza:
Wamesema uongo mwingi sana, mimi nasema tu nilichopata nimepata na sina utajiri kiasi hicho, lakini si mbadhirifu wa haki zangu ninazopata kama mshahara na haki nyingine.
Alipotakiwa kutaja mali anazomiliki, Lowassa alisema:
Mimi ni mfugaji, nina ng’ombe zaidi ya 800 jimboni kwangu Monduli.

0 comments:

Chapisha Maoni