Hospital ya rufaa ya mkoa wa Mtwara ya Ligula imelalamikiwa kwa
kukosa huduma za vipimo vya damu huku wodi ya watoto wakilazimika kulala
watoto wawili hadi wa tatu kitanda kimoja, kutokana na ukosefu wa
vitanda.
Baadhi ya wakazi wa Mtwara waliopata huduma za matibabu kwenye
hospital hiyo ya rufaa ya mkoa wa Mtwara ya Ligula wamedai,
wanapoandikiwa na daktari kwenda kupata vipimo vya damu maabara,
huambiwa waende kwenye zahanati za watu binafsi na majibu ya vipimo
hivyo warejeshe hospitalini hapo, kwa kuwa hospital hiyo ya rufaa haina
vifaa vya kupimia damu, hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa
na kuitaka serikali kuingilia kati tatizo hilo kwani linaadhiri utoaji
wa huduma bora kwenye sekta hiyo ya afya.
Alipoulizwa juu ya malalamiko hayo, kaimu mganga mfawidhi hospitali
hiyo ya rufaa ya mkoa wa Mtwara ya Ligula Dr. Joseph Mwiru amekiri
tatizo hilo lilikuwepo miezi michache iliyopita na kwa sasa limepatiwa
ufumbuzi, na kuhusu wodi ya watoto kujaa na watoto kulazimika kulala
wawili hadi watatu kitanda kimoja,amesema hali hiyo imetokana na
magonjwa ya mlipuko kama Typhod, unaosababishwa na mabadiliko ya hali ya
hewa.
0 comments:
Chapisha Maoni