Arsenal watakamilisha usajili wa mshambuliaji
kutoka Chile, Alexis Sanchez, 25 anayechezea Barcelona siku ya Jumatano,
kwa mujibu wa Arsene Wenger (Talksport), Tottenham wametoa dau jipya na
'kuuteka' mchakato wa Liverpool wa
kumsajili kiungo wa Lille Divock Origi (Daily Mirror), Juventus
wamewasilisha tena dau la pauni milioni 2 kumsajili beki wa Manchester
United Patrice Evra, 33 (daily Mail), Iwapo Evra atakwenda Turin,
kiungo kutoka Chile, Arturo Vidal, 27, huenda akaweza kwenda Old
Trafford kwa kitita cha pauni milioni 32 (Daily Express), mshambuliaji
wa zamani wa Arsenal Eduardo, 31, amewaaga wachezaji wenzake wa Shaktar
Donetsk huku kukiwa na taarifa kuwa atajiunga na Flamengo ya Brazil (Sky
Sports), Roma na Napoli za Italia pamoja na mabingwa wa Ubelgiji
Anderlecht wamepanda dau kumsajili beki wa kulia wa Marekani DeAndre
Yedlin, 21, ambaye aliichezea Seattle Sounders ya Marekani msimu
uliopita (Sky Sports), Paris St-Germain wapo tayari kutoa pauni milioni
70 kumnunua kiungo mfaransa Paul Pogba, 21, kutoka Juventus (Le Figaro),
Juventus pia wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro
Morata, 21 (Marca) mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba, 36,
anasuburi huenda Juventus wakamuita baada ya kumaliza mkataba wake na
Galatasaray ya Uturuki (Tuttosport), Arsenal wanakaribia kupata saini ya
Loic Remy kutoka QPR. Timu hizo mbili karibu zinakamilisha makubaliano
juu ya ada ya uhamisho, ingawa Remy bado hajazungumzia maslahi binafsi
na Gunners (Daily Mirror), baada ya kukamilisha mikataba ya Alexis
Sanchez na Mathiew Debuchy, mchezaji mwingine anayesakwa na Arsenal ni
kiungo wa Real Madrid Sami Khedira. Los Bloncos watamruhusu Khedira
kuondoka baada ya kufanikisha uhamisho wa Toni Kroos (Daily Express),
Manchester United wanajiandaa kumnyatia Ricardo Rodriguez anayechezea
Wolfsburg, kuziba nafasi ya Patrice Evra (Magazeti mbalimbali), Atletico
Madrid wamekubaliana na Bayern Munich juu ya Mario Mandzukic kwa kitita
cha euro milioni 22 (Bild), Everton wanataka kumsajili kwa mkopo Demba
Ba kutoka Chelsea (Daily Star), Niklas Bendtner anatarajiwa kusaini
katika timu mpya wiki hii baada ya kuruhusiwa kuondoka na Arsenal (BBC)
na winga wa Manchester United, Adnad Januzaj, 19, amepata vitisho
kufuatia uamuzi wake wa kuichezea Ubelgiji badala ya Albania au Kosovo,
kwa mujibu wa taarifa kutoka Serbia (Daily Mail).




0 comments:
Chapisha Maoni