Kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal angependa kumchukua
Wesley Sneijder, 30, kutoka Galatasaray, lakini klabu hiyo ya Uturuki
inataka pauni takriban milioni 6 (Sun), Liverpool watamuuza Luis Suarez,
27, kwenda Barcelona mwisho wa wiki hii, ikiwa klabu hizo zitakubaliana
ada ya pauni milioni 75 (Daily Mirror), Lakini Arsenal wamekasirishwa
kwa sababu jaribio lao la kumchukua Alexis Sanchez, 25, kutoka Barcelona
linacheleweshwa kutokana na mkataba wa
Suarez kudemadema (Daily Express), Arsenal wanataka kulipwa pauni
milioni 6 kumuuza Mikel Arteta, 32, kwenda Fiorentina (Times), Roma
wamewapa Manchester City hadi tarehe 21 mwezi huu wawe wamekamilisha
usajili wa beki wa kati kutoka Morrocco Mehdi Benatia, 27, (Guardian),
Chelsea wanamsajili beki wa kulia wa Atletico Madrid, Luis Filipe, 28,
kuziba nafasi ya Ashley Cole aliyekwenda Roma (Sun), winga kutoka
Colombia Juan Cuadrado, 27, huenda akahamia Manchester United kutoka
Fiorentina (London Evening Standard), mshambuliaji wa Liverpool Iago
Aspas, 26, anajiandaa kuhamia Sevilla, baada ya kushindwa kupata namba
Anfield (Daily Star), Brendan Rodgers pia anafikia kutoa pauni milioni
10 kumchukua beki wa kushoto wa Swansea Ben Davies, 21 (Daily
Telegraph), Manchester United, Liverpool, Chelsea na Arsenal zitapambana
kupata saini ya winga wa Benfica Joao Filipe anayetajwa kuwa "Cristiano
Ronaldo mwingine" pamoja na kipa Joao Virginia, wote wana umri wa miaka
15 (Daily Express), Manchester United wanafikiria kumsajili beki wa
kushoto wa Wolfsburg na Uswisi, Ricardo Rodriguez, 21, kuziba nafasi ya
Patrice Evra ambaye huenda akahamia Juventus (Times), Lakini Louis van
Gaal pia huenda akamchukua beki Daley Blind, 24, kutoka Feyenoord ikiwa
Evra ataondoka (Manchester Evening News), kiungo kutoka Nigeria Michael
Babatunde, 21, anayechezea Volyn Lutsk nchini Ukraine, amedai kuwa
Sunderland wanataka kumsajili (Newcastle Chronicle), Bayern Munich
wamesema wamefikia makubaliano yasiyo ya maandishi na Atletico Madrid ya
kumsajili Mario Mandzukic, 28 (Marca), mshambuliaji wa Real Madrid
Alvaro Morata huenda akajiunga na Juventus mapema wiki ijayo
(Tuttosport), na hatimaye, kinyozi wa Alexis Sanchez amethibitisha kuwa
mchezaji huyo anahamia Arsenal! (Metro). Share tetesi hizi na wapenzi
wote wa soka. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.




0 comments:
Chapisha Maoni