Liverpool wapo tayari kumfuatilia tena Ryan
Bertrand, 24, kutoka Chelsea, wakati Brendan Rodgers akisaka beki wa
kushoto (Daily Mail) kiungo wa Borussia Dortmund Marco Reus, 25, na beki
wa Southampton Dejan Lovren, 25, ni miongoni mwa wachezaji Brendan
Rodgers anawafuatilia (Daily Mirror) Everton wanakaribia kumsajili
Muhamed Besic, 21, kutoka Bosnia (Daily Mirror), Tottenham wanafikiria
kumtaka beki Ron Vlaar, 29, wa Aston Villa, na wapo tayari kubadilishana
na Lewis Holtby au Michael Dawson (Daily Mail), Chelsea wanamfuatilia
kwa karibu beki Rafael Varane kutoka Real Madrid (Independent),
Liverpool wana matumaini ya kuuteka mchakato wa uhamisho wa kiungo wa
Juventus Arturo Vidal, 27, kwa kutoa dau la pauni milioni 42.5 walizotoa
Manchester United (Metro), meneja wa Everton Roberto Martinez
amethibitishwa kuwa anakaribia kumsajili David Henen, 18, kutoka
Anderlecht (Talksport), AC Milan wanamfuatilia mshambuliaji wa Arsenal,
Joel Campbell, 22, na tayari wamewasiliana na klabu hiyo ya London
(Inside Futbol) Louis van Gaal anakabiliwa na mtihani mgumu baada ya
Borussia Dortmund kumuonya kuwa asahau kumsajili Mats Hummels, 25 (Daily
Express), Manchester United 'wameruhusiwa' kumsajili winga wa Real
Madrid Angel Di Maria, 26, baada ya timu hiyo kumsajili James Rodriguez
kutoka Monaco (Caughtoffside) hata hivyo taarifa nyingine zinasema Di
Maria anataka kwenda PSG kwa mkopo kwanza kabla ya uhamisho wa kudumu
msimu ujao (Daily Express), boss wa Chelsea Jose Mourinho amewaambia
makipa wake, Thiabaut Courtois, 22, na Petr Cech, 32, kuwa hawaendi
popote, watake wasitake (Times), Arsene Wenger yuko tayari kuacha
kutafuta kiungo mwingine, na atamuamini Jack Wilshere, 22 (Daily
Mirror), boss wa QPR, Harry Redknapp anataka kumsajili mshambuliaji wa
zamani wa Chelsea Samuel Eto'o (Daily Mirror) Romelu Lukaku wa Chelsea,
21, anakaribia kuondoka Darajani baada ya kufanya mazoezi na klabu yake
ya zamani Anderlecht (Sun).
0 comments:
Chapisha Maoni