Jumatano, Julai 23, 2014

SHULE ZILIZOFELISHA KIDATO CHA SITA KUTOA MAELEZO

SHULE zote za Serikali zilizofanya vibaya katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka huu 2014, ambazo mazingira na nafasi yake iliruhusu kufanya vizuri, zimeamriwa kujieleza sababu za kufanya vibaya.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Jumanne Sagini amesema Makatibu Tawala Mkoa, wameagizwa kutoa maelezo na kufanya utafiti ndani ya mwezi kubaini sababu za shule hizo kufanya vibaya ili hatua stahiki zichukuliwe, hali hiyo isijirudie.

0 comments:

Chapisha Maoni