Alhamisi, Julai 31, 2014

MAKUBWA YALIYOTOKEA IRINGA

Watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Iringa kwa tuhuma mbalimbali ikiwepo ya mtu mmoja kushikiliwa kwa tuhuma ya kumpiga kisha kumjeruhiwa mtoto wake kwa kitu chenye ncha kali.
Kamnda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema Nelson Mdakilwa umri miaka 48 mkazi wa kijiji cha Isele wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumpiga kwa makofi na mateke kisha kumjeruhi mtoto wake Isaka Mdakilwa umri miaka 17 kwa kitu chenye ncha kali.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa mtoto huyo ni mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Isele na kabla hajamfanyia unyama huo mtuhumiwa alimfunga mikono kwa kamba chanzo kikiwa ni kumtuhumu kuwa amekataa kwenda shule.
Aidha amesema jeshi la polisi wakiwa doria wamemkamata Kristiani Godelo umri miaka 35 mkazi wa eneo la ILula Sokoni wilaya ya Kilolo mkoani Iringa akiwa na bhangi kete 80 ambapo mtuhumiwa huyo ni muuzaji na mtumiaji bhangi hizo.
Hata hivyo Kamanda Mungi amesema ushirikiano wa wananchi na jeshi la polisi kumepelekea kipindi cha sikuku kuwa katika hali ya utulivu ambapo kumetokea vifo vya watu wawili ikiwepo ya mtu mmoja kufariki wakati akiendelea na matibabu katika hospitari ya Mkoa Iringa baada ya kuanguka wakati wa dua uwanja wa Samola.

0 comments:

Chapisha Maoni