LICHA ya Jeshi la Polisi nchini, kushindwa kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa wa madawa ya kulevya katika mkoa wa Arusha, Polisi mkoani humo kwa kushirikiana na Askari wa Kampuni ya Jumuiya ya Jamii, wamefanikiwa kukamata magunia 20 ya dawa za kulevya aina ya bangi yaliyotelekezwa kwenye Kijiji cha Olteres wilayani Longido mkoani humo.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas,amesema Julai 25, 2014 kwamba tukio hilo lilitokea jana Julai 24, 2014 saa 20:30 usiku wakati Askari wa Jumuiya ya jamii wanaofanya ulinzi wa kulinda wanyamapori na mazingira katika Kambi ya Enduimet wakiwa doria waliona magunia hayo yakiwa yametelekezwa baada ya watuhumiwa kuhisi wanafuatiliwa. Watuhumiwa walipoona wanaweza kukamatwa waliamua kufungua magunia hayo ya bangi iliyokuwa imebebwa na wanyama aina ya Punda ambao mara nyingi huwatumia kusafirisha mizigo yao na kutokomea kusikojulikana
alikaririwa Kamanda Sabas.
Alisema baada ya kupata taarifa za kuwepo watu wanaosafirisha bangi kupitia njia za ‘Panya’walianza kuwafatilia lakini hawakuweza kuwakamata kutoka na kubaini mtego huo na kuwa Jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu hao. Alifafanua kuwa watu hao walikua wakitokea maeneo ya Oldonyosambu wilaya ya Arumeru kuelekea Namanga katika mkoa huo na kuwa walikuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa walisafirishaji walikuwa wakielekea nchi jirani ya Kenya ambako inadaiwa kuwepo kwa soko la bidhaa hiyo iliyopigwa maarufuku hapa nchini.
0 comments:
Chapisha Maoni