Alhamisi, Julai 03, 2014

MADEREVA TAXI WA KIGENI WAPIGWA MARUFUKU SUDAN KUSINI

Madereva wa taxi kutoka Sudan wanaofanya kazi Sudan Kusini wamekasirika baada ya raia wa kigeni kupigwa marufuku kufanya kazi. Wizara ya mambo ya ndani ilitoa tangazo wiki iliyopita, bila onyo lolote, kwa mujibu wa madereva wenye hasira wakizungumza na Radio Tamazuj.
Wamesema maafisa wanayakamata magari yao mjini Juba na kudai kiasi cha dola 150 ili yaachiliwe. Madereva wapatao 500 kutoka Sudan wamelazimika kuacha kazi, na sio tu kuathiri maisha yao, bali pia kuzua sokomoko la usafiri mjini Juba.
Sudan Kusini pia ilipiga marufuku raia wa kigeni kuendesha bodaboda mwaka jana, kwa madai kuwa zinachochea utekaji nyara, wizi wa mifukoni na ajali za barabarani. Wachambuzi wengi wamesema ilikuwa njia ya kuleta ajira kwa wenyeji. Watu kutoka Uganda, Kenya na Sudan walifurika Sudan Kusini mara baada ya nchi hiyo kupata uhuru wake mwaka 2011. Ubalozi wa Sudan umeahidi kuwasaidia madereva hao, ingawa haijasema lolote zaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni