Wafuasi wa dini tukufu ya Kiislamu katika nchi za Iraq, Uturuki, Qatar,
Misri, Saudi Arabia na Bahrain leo wanasherehekea sikukuu ya Idul Fitr
baada ya kumalizika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Taarifa
zinasema kuwa, katika nchi nyingine kama vile Umoja wa Falme za Kiarabu,
Jordan, Kuwait, Yemen, Syria, Lebanon, Afghanistan, Tajikistan,
Kazakhstan na Palestina leo Jumatatu ni tarehe Mosi Shawwal. Hali
kadhalika, Waislamu nchini Rwanda leo wanasherehekea sikukuu ya Idul
Fitr. Hata hivyo, nchi nyingi duniani zimetangaza kuwa, sherehe za
sikukuu ya Idul Fitr zitafanyika kesho Jumanne. Nchi kama vile Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran, Pakistan, Tanzania na Azerbaijan zimetangaza kuwa
sherehe za Idul Fitr zitafanyika kesho.
0 comments:
Chapisha Maoni