Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi (Veta) imevumbua boti
inayojiendesha bila nahodha ambayo ina uwezo wa kutuma taarifa za
kijasusi na kujilinda dhidi ya mashambulizi au uharibifu unaoweza
kufanywa na watu wenye nia mbaya.
Akizungumza wakati wa Maonyesho ya 38 ya Biashara
ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) katika Viwanja vya Mwalimu Julius
Nyerere jijini hapa jana, Mvumbuzi wa mashine hiyo, Immanuel Bukuku
alisema kuwa imemchukua miezi sita kufanikisha uundaji wa mashine hiyo.
Alisema uvumbuzi huo umeambatana na majaribio
ambayo yamefanyika katika Pwani ya Kigamboni na yameonyesha mafanikio
makubwa na ipo tayari kwa ajili ya matumizi ikiwa na kamera za kutosha
kwa ajili ya uchunguzi na kupeleka taarifa.
Uvumbuzi umekamilika na boti ipo tayari kwa ajili ya matumizi na wadau wanakaribishwa kwa ajili ya kusaidia ufanikishaji wa utengenezaji wa boti nyingine zaidialisema na kuongeza kuwa boti hiyo itakuwa inaongozwa na mashine nyingine itakayo kuwa sehemu maalumu.
Bukuku ambaye ni mwalimu wa masuala ya Sayansi na
Teknolojia katika Chuo cha Veta Chang’ombe alisema amevumbua boti hiyo
ambayo imetengenezwa kwa kutumia vifaa rafiki na mazingira ya bahari na
inatumia mfumo wa umeme jua na mashine za kuzalisha umeme.
Ina uwezo wa kuhisi kuwapo kwa mtu au chombo kingine jirani yake na kutoa taarifa katika sehemu ambako kinaratibiwa, pia ina uwezo wa kushambulia kwa kutumia mitutu na ina uwezo mkubwa katika masuala ya ulinzi na usalamaalisema.
Alisema pia amefanikiwa kutengeneza injini ya
ndege ambayo imeonyesha mafanikio kwa kiasi kikubwa na wakati wowote
inaweza kutumika na mafanikio hayo yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na
mpango wa Veta wa kuwa na Kitengo cha Masuala ya Ufundi na Ubunifu.
Kuna mashine na teknolojia nyingi ambazo zimevumbuliwa hapa, ni dalili njema na tuna matumaini kuwa uvumbuzi zaidi unafuata kutokana na tafiti nyingi kuonyesha dalili za mafanikioalisema na kuongeza kuwa kitengo hicho kimepania kubadili mwelekeo mzima wa Veta kwa hivi sasa.
0 comments:
Chapisha Maoni