Wakati Tanzania ikiendelea kuneemeka kwa ugunduzi wa rasilimali nyingi
za asili ikiwamo gesi asilia, hivi karibuni wenye magari wataanza
kunufaika na matumizi ya rasilimali hiyo kwa ajili ya kuendeshea vyombo
hivyo.
Hayo yalibainishwa jana na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya 38 katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika banda la TPDC, mmoja wa wafanyakazi wa
shirika hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa vile siyo msemaji,
alisema, matumizi ya gesi hiyo kwa ajili ya kuendeshea vyombo vya
usafiri yataanza jijini humo kwa vituo 12 vya majaribio ambavyo mchakato
wake unatarajia kuanza hivi karibuni baada ya kupatikana kwa mshauri
atakayemsimamia mkandarasi kwa ajili ya teknlojia hiyo.
Kwa mujibu wake, matumizi ya gesi asilia kwenye vyombo hivyo, kutawapunguzia gharama waendeshaji wa magari kwani kilogramu moja ya nishati hiyo inayouzwa kwa Shilingi 1240 inaweza kutumika kuendeshea umbali wa Kilometa 14 hadi 16 tofauti na yule anayetumia mafuta ya petroli kwani huweza kutumia lita moja kwa Shilingi 2000 kwa umbali wa kilometa sita hadi nane.
Aliongeza kuwa, gari linalotumia gesi hiyo, mtungi wake huwekwa ndani yake nyuma ya gari kwa kulazwa na kwamba ikiisha njiani, dereza anaweza kubadilisha na kutumia mafuta kama kawaida.
Alitaja faida nyingine ya kutumia nishati hiyo ni kupunguza athari kwa mazingira na kwamba katika hatua za mwanzo za majaribio, na kwamba huduma ya kubadilisha mfumo huo kutoka kutumia mafuta kwenda ule wa gesi asilia, inapatikana katika Taasisi ya Teknolojia jijini Dar es Salaam (DIT) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Bico.

0 comments:
Chapisha Maoni