Alhamisi, Julai 10, 2014

KAMA NI WEWE UTAFANYAJE?

Juma ni mwajiriwa wa kampuni fulani hapa Dar es Salaam. Ijumaa Bwana Juma alipata safari ya kikazi kwenda Arusha.
Kufika akaamua kumtafuta mpenzi wake wa siku nyingi ili apate pa kujificha, basi kesho yake mrembo akamuomba ampe laki 3.
Juma akampa A.T.M Kadi na Password na kumwambia atumie
vyovyote anavyotaka, maana anajua kabakiza elfu 5 tu kwenye akaunti ya benki
Kabla hajashitukiwa Juma akapanda gari haraka ili arudi Dar, njiani simu ikakata chaji, kufika home kaweka kwenye chaji akalala.
Asubuhi anawasha simu na sms kutoka kwa bosi wake inaingia ikisema:-
"Juma nimeweka milioni 10 kwenye akaunti yako ya benki,
usirudi kwanza Dar mpaka uwalipe mafundi".
Ungekuwa wewe ndio juma ungefanya nini?

0 comments:

Chapisha Maoni