Jumatano, Julai 02, 2014

JINSI DEMU WA CHRIS BROWN, KARRUECHE ALIVYOMSHOBOKEA DIMOND PLATNUMZ KATIKA BET

Katika hali ya kushangaza, mwanamitindo maarufu Marekani ambaye ni mchumba wa Chris Brown, Karrueche Tran alionekana kumshobokea Diamond mara alipokutana naye uso kwa uso.
Karrueche alijikuta hajiwezi alipokuwa  akimhoji Diamond ambapo moja kwa moja alimvutia kipaza sauti na kuanza kumpiga maswali huku akionesha kuvutiwa naye kwa muonekano aliokuwa nao.Karrueche alikuwa akijichekeshachekesha huku akimhoji kuhusiana na mwanamuziki ambaye Diamond anamkubali ambapo alijibu ni Chris Brown, wote wakajikuta wakiangua kicheko.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Karrueche muda wote aliendelea kumshangaa na mwisho wa siku wakabadilishana namba za simu.

0 comments:

Chapisha Maoni