Jumatano, Julai 02, 2014

HIJAB YAPIGWA MARUFUKU UFARANSA

Mahakama ya haki za binadamu barani Ulaya imeamrisha kuendelea kutekelezwa hukumu ya kupiga marufuku vazi la hijab linalofunika uso mzima nchini Ufaransa.
Kesi hiyo iliwasilishwa na mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka ishirini na nne raia wa Ufaransa ambaye alidai kuwa marufuku hiy inakiuka haki zake za kuabudu na kujieleza.
Mahakama hiyo hata hivyo imsisitiza kuwa Ufaransa inayo haki ya kuhifadhi utangamano na usawa katika jamii kwa kuweka marufuku hiyo.
Sheria hiyo iliwekwa nchini Ufaransa miaka minne iliyopita na tangu hapo Ubelgiji imeiga.

0 comments:

Chapisha Maoni