Alhamisi, Julai 24, 2014

FUTA ITIKADI ZA KIDINI, TOA MSAADA

Wananchi Mkoani Iringa wameaswa kuondoa masuala ya itikadi ya dini na siasa ili kuweza kuwasaidia Watu wasiojiweza.
Mbunge wa Iringa Mjini Mhe.Mchg.Peter Msigwa amesema wakati akitoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu katika Chuo cha dini ya Kiisilamu kilichopo kitanzini manispaa ya Iringa ambapo amesema ametoa mahitaji hayo kwa kutambua hali ya vijana hao.
Mhe.Msigwa amesema wahitaji ni wengi lakini wanajaribu kutoa kiodogo kila mahali ili kuweza kuwafikia Watu wote na vitu ambavyo vimetolewa ni pamoja na Sukari,Mafuta ya kupikia,tende na unga wa ngano.
Kwa upande wake Omari Nzowa mdhamini wa chuo hicho amesema msaada huo ni mfano kwa viongozi wengine wa Serikali na Taasisi mbalimbali nchini.
Nao baadhi ya waumini wa dini hiyo wamesema wanashukuru kwa msaada huo kwani ni ahadi ambayo ilitolewa na Mbunge tangu mwaka jana kuwa atakuwa anasaidia vituo hivyo mwaka hadi mwaka.
Hata hivyo Mkuu wa kituohicho Hasan Mohamed amesema msaada huo utasaidia Watoto yatima na wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho  ili kuwajengea msingi mzuri wa kusoma.

0 comments:

Chapisha Maoni