Askari wa uhamiaji wamewakamata watu 14 katika maeneo ya Msasani
jijini Dar es Salaam kutoka nchini India na Nepal ambao ni wahanga wa
biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu ambapo watu hao wameingia
nchini kinyume na taratibu za uhamiaji.
Kati ya watuhumiwa 14 watuhumiwa 12 ni wasichana
ambao waliletwa nchini kwa lengo la kufanya maonyesho ya nyimbo za asili
lakini wakajikuta wakingizwa katika biashara zingine ikiwemo kucheza
muziki katika nyumba za burudani.
Kwa upande mtu anayedaiwa kuwaleta wasichana hao
amesema amewaleta kwa lengo la kufanya maonyesho ya muziki huku akipinga
kuwa wasichana hao hawatumii kinyume na hivyo.
Naye mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mikoroshini
msasani amewataka wakazi wa eneo hilo kujiepusha na tabia ya kukaa na
wageni bila ya kutoa taarifa mamlaka husika.
Akithibitisha tukio hilo mkaguzi wa uhamiaji Bw
Dotto Romana amesema wanawashikilia watu hao na watachukua hatua
kulingana na mahitaji ya sheria.
0 comments:
Chapisha Maoni