Kitengo cha utendakazi cha askari polisi Nchini Kenya kimekumbwa na shida ya ukosefu wa makazi.
Hali imekuwa mbaya sana katika ski za hivu punde
kiasi ya kuwa maafisa wa kike na wenzao wa kiume, wamelazimika kutumia
kwa pamoja vyumba vyao vichache.
Hili limetokea baada ya zaidi ya
maafisa wapya 7,000, kuingizwa katika kitengo hicho miezi miwili
iliyopita na kuiongeza idadi ya maafisa wa polisi nchini Kenya kwa
asilimia 10.
Hali inaweza zidi kudorora mwaka ujao ikiwa
vyumba vipya havitapatikana kwa haraka kwani maafisa wengine 10,000
wataapishwa kujiunga na Idara ya polisi kuhuidumia wananchi na kulinda
usalama .
Mpango huo wa kupanua kitengo hicho,
ulizinduliwa bungeni na katibu wa fedha Henry Rotich alipoisoma bajeti
ya mwaka 2014/2015, juma lililopita.
Katika taarifa ya makamanda
wa majimbo iliyoonyeshwa wanahabari, maafisa waliamrishwa kuwakaribisha
wenzao wapya katika vyumba vyao wanamoishi pamoja na familia zao.
Hii inamaanisha kuwa kurutu anakaribishwa kwa chumba anakoishi Askari na mkewe na familia yake .
“maafisa wengine wanawazuia maafisa hawa wageni kuingia katika nyumba zao na kusababisha hali ngumu kwao.
Maafisa wa polisi watakaokiuka amri hiyo watachukuliwa hatua za kinidhamu . Taarifa hiyo ilisema.
Maafisa waliozungumza na wanahabari, kwa
masharti ya kutotajwa walisema kuwa amri hiyo itawanyima faragha na wake
zao mbali na kuibua uhasama na ugomvi katika familia zao.
Mgogoro huo uliwalazimisha maafisa hao wapya
kutafuta makao katika vibanda viliyo katika vituo vya polisi kwa hofu ya
kuvunja nyumba za wenzao .
Maafisa hawa wapya walitawazwa kuwa makonstebo
mwezi Aprili na kuchukuliwa katika vitengo vya Polisi ,Kitengo cha Jinai
na kikosi cha kupambana na ghasia.
0 comments:
Chapisha Maoni