Mji wa Mtwara umekubwa ghafla na ukosefu wa mafuta ya petrol kwa siku
ya 2 na kuadhiri huduma za usafiri na usafirishaji hasa usafiri wa
kutumia bodaboda, huku hofu ikitanda ya kuibuka kwa bei ya ulanguzi ,
kutokana na ukosefu huo.
Fichuo ilishuhudia vituo vingi vya kuuzia mafuta mjini
mtwara havina petrol na kukuta kwenye kituo kimoja tu kukiwa na foleni
ndefu ya waendesha bodaboda na magari, wateja wengine wakija na madumu,
na walipoulizwa wamelalamika kuwa, ukosefu huo ni mbinu za
wafanyabiashara wa mafuta kutaka kuwalangua, kwani hakuna sababu zo zote
za kutokea kwa ukosefu huo wa petrol, ikizingatiwa mawasilino wa
barabara kati ya dar es salaam na mtwara yameimarika, na hivyo
wameitaka serikali, kuingilia kati tatizo hilo, kwani kupitia biashara
ya boda boda vijana wengi wameweza kujipatia ridhiki.
Kwa upande wake meneja wa kituo cha mafuta cha
Gapco Ally Mpunjo amekiri mji wa Mtwara kukubwa na ukosefu mkubwa wa
mafuta ya petrol kwa siku 2 sasa, lakini akakanusha kuwa hali hiyo ni
mbinu za wafanyabiashara, badala yake amedai, imetokana na kuongezeka wa
wateja wa petrol hasa bodaboda ukilinganisha na uwezo wa vituo vya
mafuta vilivyopo, huku akitolea mfano kituo chake hicho wastani wa
bodaboda zinazotia mafuta kwa siku ni kati ya 400 na 500.
0 comments:
Chapisha Maoni