Jumatano, Juni 25, 2014

TUNDU LISSU:TUNAPOSEMA WATANZANIA WAGAWIWE SEHEMU YA MAPATO YA GESI NA MAFUTA MOJA KWA MOJA MSITUBEZE

Utafiti unaonyesha wazi kuwa njia ya haraka ya kupunguza umaskini ni kuwagawia wananchi wenye kipato kidogo fedha taslimu.
Mexico na Brazil wamefanikiwa kupunguza athari za umaskini kwa kuwagawia familia maskini fedha taslimu kwa masharti ya kuwapeleka watoto wao Shule wapate elimu na kuwapeleka kwenye vituo vya afya wapate chanjo na tiba.
Utafiti unaonyesha kwamba hata bila masharti, familia maskini wanatumia ongezeko la kipato kuboresha lishe ya familia, kuwaelimisha watoto na kutunza afya zao.
Kutumia mapato ya gesi na madini mengine kuwagawia Wananchi kutaongeza kasi ya kutokomeza umaskini Nchini
Mpango wa kugawa fedha za maliasili sio nadharia tu, kwani tayari unatumiwa na baadhi ya Serikali.
Jimbo la Alaska, Marekani wana mfuko wa gesi na mafuta, ambapo mapato ya mfuko huu yanagawiwa kwa wananchi.
Mongolia wanatumia sehemu ya mapato yatokanayo na madini ya Shaba na Dhahabu kulipa ruzuku kwa watoto wote wa Mongolia, na Bolivia wanatumia sehemu ya mapato ya gesi kuwalipa pensheni Wazee wote wa Nchi hiyo.
Nukuu katika aya hizo mbili, nimeitoa katika hotuba ya Prof.Lipumba aliyoitoa wakati akifungua Mkutano wa Sita wa Chama Cha Wananchi (CUF) Jumatatu 23, June 2014.

0 comments:

Chapisha Maoni