Alhamisi, Juni 19, 2014

TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA

Siku kama ya leo miaka 137 iliyopita, chombo cha kwanza cha kupaa angani, kilifanyiwa majaribio ya kutua au kubakia angani bila ya kuhitajia uwanja wa kutua. Chombo hicho ambacho kilipewa jina la helikopta, kilifanyiwa majaribio na Enrico Forlanini, mhandisi wa Kitaliano katika bandari ya Alexandria nchini Misri.

Siku kama ya leo miaka 63 iliyopita inayosadifiana na 29 Khordad 1330 Hijria Shamsia, baada ya kupitishwa sheria ya kutaifisha mafuta nchini Iran tarehe 29 Esfand 1329 Hijria Shamsia, jopo lililoundwa la wataalamu wa Kiirani, lilipewa jukumu la kuliongoza Shirika la Taifa la Mafuta la Iran. Jopo hilo liliundwa kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na Ayatullah Kashani na Dokta Muswaddiq, na kupitishwa na Bunge na hatimaye Baraza la Seneti hapa nchini.

Na siku kama ya leo miaka 37 iliyopita inayosadifiana na 29 Khordad 1356 Hijria Shamsia, alifariki dunia Dakta Ali Shariati, mwandishi na msomi wa Kiirani wa zama hizi mjini London, Uingereza. Baada ya kumaliza masomo yake ya juu, Dakta Ali Shariati aliingia kwenye uwanja wa siasa na kupambana dhidi ya utawala wa kifalme hapa nchini. Msomi huyo ameacha athari za vitabu kadhaa, miongoni mwa hivyo, ni Historia ya Ustaarabu', Uislamu na Mwanadamu' na Fatima ni Fatima.'

0 comments:

Chapisha Maoni