SERIKALI imewatahadharisha wananchi wanaotumia dawa za kuongeza maumbile kwa jinsia zote kuacha mara moja kufanya hivyo, kutokana na madhara makubwa ya kiafya yanayosababishwa na dawa hizo kwa watumiaji.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Steven Kebwe, ametoa kauli hiyo Bungeni mjini Dodoma leo Jumanne, Juni 24, 2014 na kusema kuwa dawa hizo zinazotumiwa na wanawake kuongeza makalio pamoja na kukuza maumbile kwa wanaume zinasababisha ulemavu na kwamba serikali haitatoa fidia kwa wanaoathirika na dawa hizo.
Mtumiaji anaweza kuathirika kwa mfano kama ni mama, kalio moja linaweza kuwa dogo na titi linaweza kuwa kubwa na lingine dogo; na akina Baba wakati mwingine umbile lao linaweza kuwa kama mkufu. Tunatoa kauli kali kwa watumiaji waache tabia hiyo mara moja kwani suala la kulipa fidia si jukumu la serikali kwa sababu ni utaratibu ambao mtumiaji anatumia kwa hiari yake bila kuishirikisha serikali
alikaririwa na Fichuo.
Amesema kulingana na sheria inayotumiwa na serikali namba (1) ya mwaka 2003 ya Mamlaka ya Chakula la Dawa na vipodozi hairuhusu kutumia dawa hizo, hivyo watu wanaotumia dawa hizo wanatakiwa kuacha mara moja ili kuepuka madhara makubwa yatokanayo na dawa hizo.
Aidha, amewataka watu wanaoingiza dawa hizo nchini kuacha mara moja na kuahidi kuwa serikali itawachukulia hatua kali wote watakaobainika kuingiza dawa hizo kinyemela au kwa njia yoyote, kutokana na agizo hilo kupuuzwa na baadhi ya wafanyabiashara wanaouza dawa hizo.
Fichuo imebaini kuwa katika kipindi cha mwaka jana Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, National Health Insurance Fund (NHIF), ulisema hautahusika na malipo ya matibabu kwa wanachama wao watakaoathirika na utumiaji wa dawa za kuongeza maumbile ambazo zimepigwa marufuku na Serikali.
Hata hivyo, taarifa zinasema licha ya serikali kupiga marufuku utumiaji wa dawa hizo bado wananchi wengi wamekuwa wakitumia dawa hizo bila kuzingatia kanuni na sheria za chakula dawa na vipodozi ambapo dawa za kichina zimetajwa kuuzwa kila kona na zimekuwa na athari kubwa kwa maisha ya binadamu na baadhi zimekuwa zikiongeza shinikizo la damu pamoja na athari nyingine.

0 comments:
Chapisha Maoni