Ijumaa, Juni 13, 2014

MWANAMUZIKI WA INJILI AFARIKI DUNIA BAADA YA AJALI YA NDEGE

Mwanamuziki wa muziki wa injili  aliyejishindia tuzo nyingi nchini Nigeria, Kefee Don Momoh, amefariki dunia mapema leo baada ya kuwa katika hali ya kupoteza fahamu kwa muda wa wiki nzima hospitalini alikokuwa amelazwa nchini Marekani kwa mujibu wa Fichuo TZ.
Alipoteza fahamu baada ya kuanguka toka juu ya ndege alipokuwa akielekea Chicago kwa ajili ya shoo wiki mbili zilizopita. Chanzo cha karibu na familia yake kimedai kuwa Kefee Don Momoh alikuwa na ujauzito mchanga pamoja na shinikizo la damu.
OAP Yaw, ambaye ni rafiki wa karibu wa mume wake, OAP Teddy Don Momoh alithibitisha habari kifo hicho katika redio ifahamikayo kama Wazobia Fm asubuhi ya leo akisema:

Mtu wa muhimu sana kwetu amekufa. Nafsi yake ipumzike kwa amani.
Kefeeambaye alianza kazi ya muziki akiwa na miaka nane tu katika kwaya ya kanisa yake, alikuwa maarufu kwa nyimbo zake za injili kama 'Branama' na 'Kokoroko. Alishinda tuzo kadhaa ikiwa ni pamoja na tuzo la mwanamuziki bora wa kushirikiana Collaboration Headies mwaka 2010.  
Mpaka kifo chake, alikuwa akiishi vema kwa furaha na mume wake nchini Marekani na kusimamia mgahawa wake, Branama Kitchen, katika Lagos.

0 comments:

Chapisha Maoni