Kiungo mshambuliaji mpya wa timu ya Young Africans SC Andrey Marcel
Ferreira Coutinho amewasili mchana wa leo jijini Dar es salaam akitokea
kwao nchini Brazil tayari kabisa kwa kuanza kazi ya kuwatumikia wana
Wanajangwani katika msimu wa 2014/2015.
Countinho amewasili mchana kwa shirika la Ndege la Afrika Kusini
(South African Airways) akitoka jijini Sao Paul ambapo safari ya kuja
Tanzania imemkchukua takribani masaa 20 tokea katika Mji wa Berem ambapo
ndipo anapoishi.
Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa JK
Nyerere, Coutinho alipokelewa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Bw.
Mohamed Bhinda ambaye alimuongoza kuwasilimia washabiki na waaandishi wa
habari walijitokeza kumlaki.
Akiongea na waandishi wa habari
Uwanja wa Ndege Coutinho amesema anajisikia furaha kuwa Tanzania, nchi
ambayo watu wake wanapenda mpira na kikubwa amekuja kuisaidia Yanga
kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali mbali itayakayowakabili.
Kuhusu
changamoto za ugeni katika Bara la Afrika, Coutinho alisema soka kwake
ni kazi, ana uzoefu baada ya kucheza pia Barani Asia hivyo hana
wasiwasi, na kwa kuwa na walimu aliwazoea anaamini kwa pamoja atafanya
vizuri.
Msafara wa kutoka Uwanja wa ndege ulielekea makao makuu ya
klabu mitaa ya Twiga/Jangwani ambapo Coutinho aliwasilimia wapenzi,
washabiki na wanachama waliojitokeza kumpokea, kisha aliongea na katibu
mkuu Bw Beno Njovu kabla ya kwenda kupumzika.
0 comments:
Chapisha Maoni