Alhamisi, Juni 26, 2014

MANENO YA MBOWE JUU YA CHADEMA

Hiki Chama mwanzoni kilikuwa ni Chama kilichoongozwa na viongozi na viongozi ndio walikuwa na maamuzi ya mwisho.
Leo Chama hiki kimekuwa sana, ni kimbilio la mamillioni kwa mamillioni ya watanzania.
Mimi kama Mwenyekiti na Viongozi wenzangu kama Kamati Kuu, tutatumia kila linalowezekana chini ya Katiba ya Chama kukilinda Chama hiki.

Hatutakubali mtu yeyote yule miongoni mwetu kwa sababu zake binafsi au kwa sababu alizotumwa na mtu mwingine yeyote, ili akiumize Chama hiki. Gharama ya kukivunja Chama hiki ni gharama kubwa mno, ni gharama kubwa kwa Demokrasia. Kwa hiyo ni wajibu wangu na wenzangu katika Kamati Kuu kuilinda Katiba na kukilinda Chama hiki kama mboni ya jicho.
Na nawahakikishieni ndugu Waandishi wa habari kuwa Chama hiki kiko salama na kitakuwa salama, kitaimaarika zaidi na hakitammezea mate au kumbania yeyote yule ambaye kwa njia yoyote ile anafikiri pengine anaweza kuwa na umashuhuri kuliko Chama, sio mimi Mbowe, sio Katibu Mkuu Dr.Slaa, sio Tundu Lissu au Mbunge mwingine yeyote yule.
Hiki Chama ni muhimu kuliko Kiongozi mwingine yeyote ndani ya Chama, kwa sababu Chama hiki ni mjumuiko wa mawazo, damu, nguvu, vifungo na matatizo tofautitofauti ambayo yamewakumba Watanzania wengi katika harakati za kuifikisha CHADEMA hapa ilipofika.
Hatutakubali kikundi au mbinu yoyote chafu ya kuidhoofisha CHADEMA na nawahakikishia huo ndio msingi wa CHADEMA, UWAZI na UKWELI.

0 comments:

Chapisha Maoni