ZIMESALIA siku tano tu, kuanzia Jumatano wiki hii, kabla ya baadhi ya mali za Mbunge maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kapteni John Komba, kupigwa mnada ili kufidia deni kubwa alilonalo katika Benki ya CRDB.
Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali zilizopatikana, Komba anayemiliki shule kadhaa jijini Dar es Salaam, ikiwamo ya Bakili Muluzi, anadaiwa na Benki ya CRDB zaidi ya Sh bilioni moja, ikiwa ni deni la msingi pamoja na riba ya asilimia 17 katika miaka mitano anayodaiwa kushindwa kulipa deni hilo.
Deni la msingi ni Sh milioni 900, lililotolewa katika mikupuo miwili; kwanza Sh milioni 300 na baadaye Sh milioni 600, baada ya maombi ya mkopo aliyoyatuma CRDB mwaka 2007, kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madarasa, nyumba za wafanyakazi, mabweni, uchimbaji wa visima na ununuzi wa samani kwa ajili ya madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule yake hiyo ya Bakili Muluzi.
Marejesho ya mkopo huo uliopaswa kulipwa ndani ya miaka mitano, yalitakiwa kufanyika katika mikupuo 22 na kumalizika Juni 30, 2014. - See more at:

0 comments:
Chapisha Maoni