Kwa nini Luis Suarez? ok, ni mchezaji ambaye hakuna anayetia shaka
juu ya uwezo wake dimbani lakini tabia yake ya kuuma wachezaji wenzake
pindi anahisi kuudhiwa linatia shaka na jana dhidi ya Italy Kombe la
Dunia 2014.
ILIVYOTOKEA: Italy wakiwa mchezaji mmoja pungufu baada ya Marchisio kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 59. Matokeo yakiwa 0-0, huku Italy wakiwa bado katika nafasi nzuri yakufuzu, jambo la kustaajabisha lilitokea. Luis Suarez alimuuma beki wa Italy Chiellini kwenye bega lake la kushoto na kuwafanya wachezaji wote wa Italy kushikwa na mshangao na labda kuwatoa mchezoni kifikra. Dakika moja mbele, Diego Godin aliipatia bao Uruguay lililowatoa Italy.

Ni
dhahiri, habari kubwa ilipaswa kua kutolewa mapema kwa Italy lakini
kitendo cha Suarez kuuma mtu kwa mara ya tatu imekua habari kubwa. Luis
Suarez mchezaji mahiri wa Liverpool na Uruguay si kwamba amefanya hivi
mara moja ama mbili, bali mara tatu sasa!
2010 | Alifungiwa mechi 7 kwa kosa la kumuuma mchezaji wa PSV, Otman Bakkal kipindi hicho akiichezea klabu ya Ajax.
2012 | Aliuma tena safari hii alifungiwa mechi 10 na muathirika wa meno yake alikua ni beki wa Chelsea Branislav Ivanovic.
2014 | Luis Suarez alionekana kuuma bega la Girogio Chiellini beki wa
Italy katika mashindano ya Kombe la Dunia huko Brazil. FIFA bado kuamua
adhabu ambayo atapewa.
0 comments:
Chapisha Maoni